Saturday, March 24, 2012

                         .  VIJANA WAMSHUKIA WAZIRI KABAKA
                         .  WAUNGA MKONO KAULI YA LOWASA TATIZO LA AJIRA NCHINI
                           WAZIRI WA KAZI AJIRA NA VIJANA MH,GAUDENSIA KABAKA

Na Daniel Limbe,Geita
 SIKU chache baada ya serikali kupinga vikali kauli ya aliyekuwa waziri mkuu aliyejihudhuru Edward Lowassa kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana nchini,baadhi ya vijana wilayani hapa mkoa mpya wa geita wamemshukia waziri wa Ajira kazi na vijana Gaudensia Kabaka huku wakiunga mkono kauli ya Lowasa.

Lowasa amewahi kukaliliwa zaidi ya mara tatu akitoa angalizo hilo kwa serikali na kulifananisha na bomu linalotarajiwa kulipuka siku za usoni iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuhakikisha vijana wanapata ajira.

Kufuatia hali hiyo serikali kupitia waziri wake wa kazi ajira na vijana alivunja ukimya na kupinga vikali kauli hiyo kwa madai kauli hizo ni kutoitendea haki serikali kwa kuwa inaendelea kukabiliana na tatizo hilo na kwamba imefanikiwa kupunguza tatizo la ajira kwa aslimia 1.2 kutoka mwaka 2000/1 hadi kufikia mwaka 2006.

Wakizungumza katika kongamano la vijana kuhusiana na tatizo la ajira hapa nchini lililofanyika kata ya kamena wilayani geita na kuhudhuliwa na vijana zaidi ya 1200 wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Kamena na Nyamalimbe,ambalo limefadhiliwa na shirika NELICO kupitia programu ya sauti ya vijana wamesema tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa na kwamba serikali imeshindwa kutengeneza mazingira rafiki ya kuwasaidia kujiajiri.

Wamesema serikali inaowajibu mkubwa wa kuwasaidia vijna kupata ajira rasmi na zisizo rasmi ili kupunguza ongezeko la umaskini hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufufua na kujenga viwanda vingi nchini,kutoa elimu inayoweza kumfanya kijana kuwa na ujuzi na maarifa,kutoa mikopo kwa masharti nafuu na kuwapatia pembejeo zenye ruzuku ya serikali badala ya kuendelea kuwahimiza kusoma kwa lengo la kukusanya vyeti visivyo na tija.

“Tulisikitika sana kuona serikali ikipinga kauli ya lowasa kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijna lilivyo kubwa hapa nchini,ukweli hakuna nchi inayoweza kuendelea pasipo kuwa na viwanda nchini kwake…ili kuondoa tatizo hili kunahaja kubwa kwa serikali kuimalisha na kujenga viwanda,kutoa mikopo kwa masharti nafuu,na kutupa vijana hasa tulioko vijijini pembejeo za kilimo tena kwa wakati ili tusaidie kukuza uchumi wan chi badala ya kundelea kukusanya vyeti”alisema Richard Poleni.

Na kwamba njia nyingine ya kusadidia kuondoa tatizo hilo ni serikali kupunguza mishahara na posho za viongozi wa ngazi za juu ili kuiwezesha kuwa na pesa za kuajili vijana wengi ambao humaliza elimu zao na kukosa kazi hali inayosababisha baadhi yao kujiingiza kwenye vitendo vya ujambazi na uporaji.

Kadhalika katiba ya nchi ibadilishwe na kutambua uwepo wa ajira kwa vijana badala ya kuendelea na utaratibu ulivyo hivi sasa ambapo vijana wamekuwa wakinyimwa kazi huku baadhi ya wazee wakiwa wameng’anga’nia madarakani na wengine kutoa ajira kwa “undugu nazesheni” hali inayowanyima vijana wengi haki ya kuajiriwa.
Kwa upande wake Alphonce Emmanuel ameitaka serikali kubadili mfumo wa utoaji elimu kwa wananfunzi huku akisisitiza masomo ya stadi za kazi na maisha vipewe kipaumbele ili kumwandaa kijana anapo hitimu elimu yake awe na uwezo wa kujiajiri mwenyewe badala ya kuendelea kusubili kuajiliwa na serikali.

Amedai kuwa serikali haiwezi kukwepa tatizo la ajira kwa vijana,ni vema ikatafuta mbinu sahihi ya kuondoa tatizo hilo badala ya kuendela kupinga uwepo wa changamoto hiyo ilihali vijana wengi wakiwa mitaani hawana ajira.

Mratibu wa kitengo cha sauti ya vijana ambaye pia ni mwana sheria wa asasi ya NELICO Benard Otieno amesema lengo la kongamano hilo limelenga kutoa wigo wa kuhakikisha sauti za vijana zinasikika kwa viongozi na watunga sera kuhusiana na mabo mbalimbali yanayowahusu kila kukicha.

Sababu nyingine ni kuwafanya vijana kutambua na kutoa ufumbuzi wa matatizo yao wenyewe kwa lengo la kutumia fulsa walizonazo kujiletea maendeleo na kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo limekuwa likiwatesa vijna wengi na kulazimika kuitupia lawama serikali iliyopo madarakani.

Naye Mkuu wa idara ya saikolojia wa NELICO,Diana Renatus ameliambia gazeti hili kuwa kutokana na tatizo la ajira kwa vijana hapa nchini kuwa mwamba usiovunjika, shirika hilo limelazimika kuendela kutoa msaada wa kuwawezesha vijana kupata elimu ya ujasiliamali ili kuboresha maisha yao na kuinua uchumi wa taifa.

 Awali akitoa ufafanuzi wa tatizo hilo kwa vijana waliohudhulia kongamano hilo mmoja wa maofisa maendeleo ya jamii wilayani geita Emma Busanji aliwataka vijana kuacha kubweteka na kungoja ajira za serikali,huku akiwahimiza kutumia raslimali walizonazo kujiajiri wenyewe.

Amesema hali ilivyo hivi sasa ni tofauti na zamani kwa kuwa awali kulikuwa na wasomi wachache na ajira zilikuwa nyingi ukilinganisha na hali ilivyo hivi sasa ambapo teknolojia za kisayansi zimechangia kupunguza kwa ajira kwa wananchi na kurahisisha kazi.

                                                                


  


No comments:

Post a Comment