Katibu tawala wa wilaya ya Biharamulo Masoud Biteyimanga akijibu baadhi ya hoja katika mjadala wa elimu ya katiba uliofanyika wilayani humo hivi karibuni PICHA na Daniel Limbe
Na Daniel Limbe,Biharamulo
Hatua hiyo imeatofasiliwa na baadhi ya wananchi kuwa ni kulinda maslahi serikali ambayo kama si kufanya hivyo maendeleo yaliyopo yasingeliweza kufikiwa na kwamba ili maendeleo ya kweli yapatikane lazima baadhi ya watu waumie kwa ajili ya wengine.
Akizungumza na baadhi ya wananchi,viongozi wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi mbalimbali za serikali na kiraia waliohudhulia kwenye mjadala wa elimu ya katiba wilayani Biharamulo mkoani kagera iliyotolewa na mtandao wa mashirika ya siyo ya kiserikali mkoani humo (Kangonet), katibu tawala wa wilaya hiyo (DAS) Masoud Biteyimanga alikiri serikali kuwabambikiza kesi baadhi ya wananchi na viongozi wa madhehebu ya dini wilayani kwake
.
Kauli hiyo ambayo haijawahi kutolewa na kiongozi yeyote wa serikali hapa nchini,imekuja huku baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakilalamikia vyombo vya dola kuwabambikizia kesi kinyume cha sheria kwa maagizo ya wakubwa wao kutoka serikalini.
Kauli hiyo ambayo haijawahi kutolewa na kiongozi yeyote wa serikali hapa nchini,imekuja huku baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakilalamikia vyombo vya dola kuwabambikizia kesi kinyume cha sheria kwa maagizo ya wakubwa wao kutoka serikalini.
Biteyimanga alikuwa amemwakilisha mkuu wa Wilaya hiyo ya Biharamulo Ernest Kahindi kwenye mjadala wa utoaji elimu ya katiba iliyokuwa ikitolewa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kagera na yale ya wilaya ya Biharamulo (Bingonet) ambayo yalifanyika katika ukumbi wa shule ya msingi biharamulo kwa ufadhili wa shirika la The Foundationi for Civil Society.
Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu ushauri na mapendekezo ya mchungaji Cosmas Lugemalila wa kanisa United Pentecoste Church (UPC) lililopo wilayani humo aliyetaka kujua iwapo serikali inao mpango wa kuingiza kwenye katiba mpya kipengele cha kuwabana watu,wakiwemo viongozi wa umma ambao wamekuwa wakiwadhihaki wao pamoja na madhehebu yao hali inayoonysha wazi kuwa viongozi wa dini kutelekezwa na serikali.
Akizungumza kwa kujiamini na bila kutafuna maneno,mbele ya mbunge wa jimbo hilo,viongozi wa asasi za kiraia,na wananchi mbalimbali waliokuwemo ukumbini hapo huku akiyakejeli madhehebu ya dini za kikristo Biteyamanga alisema,"Hii nchi ni ya amani na utulivu...inaongozwa kwa misingi ya sheria ambazo zimeainishwa kwenye katiba unaposema viongozi wa dini hawashirikishwi na wamekuwa wakitengwa na kudhihakiwa si kweli"
Akitoa mfano hai ili kuthibitisha madai hayo ya serikali kushiriki kuwabambikizia kesi wahusika ili isionekane anazungumza maneno ya uongo alisema,"Tumewahi kumkamata mchungaji mmoja huko Katahoka...huyo mchungaji kazi yake ilikuwa ni kustarehe nyumbani kwake huku akiwazuia wananchi kuchangia maendeleo...tulimkamata na kumuundia ajali (kumbambikizia kesi) na tuliopomtupa gerezani kwa sasa ametoka huko akiwa amenyooka kabisa"alisema
Hata hivyo katika kile kilichodaiwa ni kukerwa na kauli ya kiongozi huyo wa umma anayewakilisha serikali ngazi ya wilaya,Mbunge wa jimbo hilo Dk Mbasa (Chadema) hakuweza kushiriki chakula,na hata alipoulizwa sababu alikanusha madai hayo nakudai alikuwa akiwahi wapiga kura wake aliokuwa amewaacha nyumbani kwake.
No comments:
Post a Comment