MKUU WA MKOA ADAIWA KUKWAMISHA UCHUMI KAGERA
BAADHI ya wananchi wa wilaya za mkoa wa kagera wamedai kukerwa na agizo la
mkuu wa mkoa huo Kanal Mstaafu Phabiani Masawe kuwataka kusitisha shughuli zao
za kiuchumi kwa saa 4 kila alhamisi ya wiki kwa lengo la kufanya usafi wa mazingira
mkoani humo
Hatua hiyo imedaiwa kuwa kikwazo kikubwa cha uchumi kwa wananchi kutokana na
muda huo kushindwa kuzalisha mali na kulazimika kujikita katika usafi wa
mazingira mbali na kwamba shughuli za usafi hufanyika kila siku kwenye majumba
yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wananchi hao
ambao hawakuwa tayali kuandikwa majina yao, kutoka wilaya za
Bukoba,Muleba,Misenyi Karagwe, Ngara,Biharamulo na Chato wameonyesha wasiwasi
wao mkubwa katika kupunguza hali ya umaskini mkubwa uliopo hivi sasa iwapo
serikali itaendelea na msimamo huo.
Aidha wamedai kukerwa na hatua ya kuzuiwa kufunguliwa kwa maduka ya
madawa,Migahawa na huduma za usafiri mpaka kukamilika muda wa kufanya usafi,
hatua mabayo inaweza kuongeza madhara makubwa kwa binadamu ikiwa ni pamoja na
vifo baada ya wagonjwa kukosa dawa walizoamliwa kununua kwenye maduka hayo.
Hata hivyo wameiomba serikali kuwatumia viongozi wa vitongoji na vijiji
katika kukagua usafi kwa kila kaya badala ya kuwataka wananchi kusitisha
shughuli zao kwa saa nne pasipo kuzalisha mali ili hali inayoweza kuchangia
ongezeko kubwa la umaskini wa vipato.
Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa wa kagera Masawe hazikuzaa matunda baada
simu zake za mkononi kutopatikana wakati wote alipopigiwa.
No comments:
Post a Comment