Saturday, March 24, 2012

                         .  VIJANA WAMSHUKIA WAZIRI KABAKA
                         .  WAUNGA MKONO KAULI YA LOWASA TATIZO LA AJIRA NCHINI
                           WAZIRI WA KAZI AJIRA NA VIJANA MH,GAUDENSIA KABAKA

Na Daniel Limbe,Geita
 SIKU chache baada ya serikali kupinga vikali kauli ya aliyekuwa waziri mkuu aliyejihudhuru Edward Lowassa kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana nchini,baadhi ya vijana wilayani hapa mkoa mpya wa geita wamemshukia waziri wa Ajira kazi na vijana Gaudensia Kabaka huku wakiunga mkono kauli ya Lowasa.

Lowasa amewahi kukaliliwa zaidi ya mara tatu akitoa angalizo hilo kwa serikali na kulifananisha na bomu linalotarajiwa kulipuka siku za usoni iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuhakikisha vijana wanapata ajira.

Kufuatia hali hiyo serikali kupitia waziri wake wa kazi ajira na vijana alivunja ukimya na kupinga vikali kauli hiyo kwa madai kauli hizo ni kutoitendea haki serikali kwa kuwa inaendelea kukabiliana na tatizo hilo na kwamba imefanikiwa kupunguza tatizo la ajira kwa aslimia 1.2 kutoka mwaka 2000/1 hadi kufikia mwaka 2006.

Wakizungumza katika kongamano la vijana kuhusiana na tatizo la ajira hapa nchini lililofanyika kata ya kamena wilayani geita na kuhudhuliwa na vijana zaidi ya 1200 wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Kamena na Nyamalimbe,ambalo limefadhiliwa na shirika NELICO kupitia programu ya sauti ya vijana wamesema tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa na kwamba serikali imeshindwa kutengeneza mazingira rafiki ya kuwasaidia kujiajiri.

Wamesema serikali inaowajibu mkubwa wa kuwasaidia vijna kupata ajira rasmi na zisizo rasmi ili kupunguza ongezeko la umaskini hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufufua na kujenga viwanda vingi nchini,kutoa elimu inayoweza kumfanya kijana kuwa na ujuzi na maarifa,kutoa mikopo kwa masharti nafuu na kuwapatia pembejeo zenye ruzuku ya serikali badala ya kuendelea kuwahimiza kusoma kwa lengo la kukusanya vyeti visivyo na tija.

“Tulisikitika sana kuona serikali ikipinga kauli ya lowasa kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijna lilivyo kubwa hapa nchini,ukweli hakuna nchi inayoweza kuendelea pasipo kuwa na viwanda nchini kwake…ili kuondoa tatizo hili kunahaja kubwa kwa serikali kuimalisha na kujenga viwanda,kutoa mikopo kwa masharti nafuu,na kutupa vijana hasa tulioko vijijini pembejeo za kilimo tena kwa wakati ili tusaidie kukuza uchumi wan chi badala ya kundelea kukusanya vyeti”alisema Richard Poleni.

Na kwamba njia nyingine ya kusadidia kuondoa tatizo hilo ni serikali kupunguza mishahara na posho za viongozi wa ngazi za juu ili kuiwezesha kuwa na pesa za kuajili vijana wengi ambao humaliza elimu zao na kukosa kazi hali inayosababisha baadhi yao kujiingiza kwenye vitendo vya ujambazi na uporaji.

Kadhalika katiba ya nchi ibadilishwe na kutambua uwepo wa ajira kwa vijana badala ya kuendelea na utaratibu ulivyo hivi sasa ambapo vijana wamekuwa wakinyimwa kazi huku baadhi ya wazee wakiwa wameng’anga’nia madarakani na wengine kutoa ajira kwa “undugu nazesheni” hali inayowanyima vijana wengi haki ya kuajiriwa.
Kwa upande wake Alphonce Emmanuel ameitaka serikali kubadili mfumo wa utoaji elimu kwa wananfunzi huku akisisitiza masomo ya stadi za kazi na maisha vipewe kipaumbele ili kumwandaa kijana anapo hitimu elimu yake awe na uwezo wa kujiajiri mwenyewe badala ya kuendelea kusubili kuajiliwa na serikali.

Amedai kuwa serikali haiwezi kukwepa tatizo la ajira kwa vijana,ni vema ikatafuta mbinu sahihi ya kuondoa tatizo hilo badala ya kuendela kupinga uwepo wa changamoto hiyo ilihali vijana wengi wakiwa mitaani hawana ajira.

Mratibu wa kitengo cha sauti ya vijana ambaye pia ni mwana sheria wa asasi ya NELICO Benard Otieno amesema lengo la kongamano hilo limelenga kutoa wigo wa kuhakikisha sauti za vijana zinasikika kwa viongozi na watunga sera kuhusiana na mabo mbalimbali yanayowahusu kila kukicha.

Sababu nyingine ni kuwafanya vijana kutambua na kutoa ufumbuzi wa matatizo yao wenyewe kwa lengo la kutumia fulsa walizonazo kujiletea maendeleo na kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo limekuwa likiwatesa vijna wengi na kulazimika kuitupia lawama serikali iliyopo madarakani.

Naye Mkuu wa idara ya saikolojia wa NELICO,Diana Renatus ameliambia gazeti hili kuwa kutokana na tatizo la ajira kwa vijana hapa nchini kuwa mwamba usiovunjika, shirika hilo limelazimika kuendela kutoa msaada wa kuwawezesha vijana kupata elimu ya ujasiliamali ili kuboresha maisha yao na kuinua uchumi wa taifa.

 Awali akitoa ufafanuzi wa tatizo hilo kwa vijana waliohudhulia kongamano hilo mmoja wa maofisa maendeleo ya jamii wilayani geita Emma Busanji aliwataka vijana kuacha kubweteka na kungoja ajira za serikali,huku akiwahimiza kutumia raslimali walizonazo kujiajiri wenyewe.

Amesema hali ilivyo hivi sasa ni tofauti na zamani kwa kuwa awali kulikuwa na wasomi wachache na ajira zilikuwa nyingi ukilinganisha na hali ilivyo hivi sasa ambapo teknolojia za kisayansi zimechangia kupunguza kwa ajira kwa wananchi na kurahisisha kazi.

                                                                


  


Friday, March 16, 2012

WAZIRI AONYA UKARIMU KWA WAHAMIAJI HARAMU


Na Daniel Limbe,Bukoba
 
WAZIRI wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mathayo David Mathayo ameonya vikali ukarimu wa watanzania wakiwemo viongozi wa serikali kuwakaribisha wahamiaji haramu wenye makundi makubwa ya mifugo kutoka nje ya nchi kinyume cha sheria,huku akitishia kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi wa idara yake ambao watabainika kuwakumbatia wahamiaji hao kutokana na maslahi binafsi.
 
Wahamiaji hao wanadaiwa kutoka nchi za Uganda , Rwanda na Burundi ambao huingia nchini kinyume cha sheria kupitia njia za panya huku wakiwa na makundi makubwa ya mifugo nakwamba hupewa maeneo ya kuishi na baadhi ya viongozi wa serikali walioko katika mipaka ya nchi kutokana na makubaliano haramu.
 
Waziri amebainisha hayo jana mjini Bukoba muda mchache baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara yake mkoani kagera kwenye Ofisi ya mkuu wa mkoa huo Fabian Masawe ambapo alisema serikali kamwe haitakubali kuona wananchi wake wanaendelea kuteseka ndani ya nchi yao kutokana na ukatili wanaotendewa na wahamiaji haramu kutoka nchi za Rwanda,Uganda na Burundi kwa kuwa kitendo hicho ni aibu kwa taifa.
 
Aidha alishangazwa na taarifa ya mkoa huo iliyoeleza wazi kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji vilivyoko mipakani kutokuwa raia wa Tanzania na kwamba walichaguliwa kwa nguvu ya fedha kutoka kwa wahamiaji haramu wa nje yanchi kwa lengo la kuwahifadhi wahamiaji hao pamoja na mifugo yao.
 
“Kamwe serikali haitakubali kuendelea kusikia unyanyasaji mkubwa wa wananchi wake wanaofanyiwa na wahamiaji haramu wenye mifugo iliyoingia nchini kwetu kinyume cha sheria kutokana na maslahi ya viongozi wachache wasio raia waliochaguliwa kwa nguvu ya fedha ili kulinda maslahi ya wahamiaji haramu” alisema Waziri Mathayo.
 
Viongozi hao wamedaiwa kuwa mawakala wa kuwakaribisha wenzao kutoka nje ya nchi pindi wanapokuwa wamepata madaraka kisha kuwapa maeneo ya kufanyia kazi zao nchini, hali inayopelekea uvunjifu wa amani nchini.
 
“Nchi hii inaongozwa kwa sheria taratibu na kanuni..ninasema kiongozi yeyote katika idara yangu atakayebainika kushirikiana na wahamiaji hao haramu kuingiza,kuhifadhi au kutoa msaada wowote kwa nia ya kuingia nchini tutamtimua kazi mara moja”.
 
Awali katika taarifa ya mkoa wa kagera,iliyosomwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Fabian Masawe,Dk Paulin Msafili alisema mkoa huo unawahamiaji haramu 35,000 ambao wameweka makazi ndani ya misitu wakijihusisha na ufugaji mifugo,Upasuaji mbao na kuchoma mkaa kinyume cha sheria.
 
Na kwamba zaidi ya ng’ombe 200,000 zimo ndani ya misitu ya hifadhi kinyume cha sheria huku baadhi ya viongozi wa serikali wakiendelea kuwakumbatia kutokana na maslahi binafsi.
 
                                                                           Mwisho.

Monday, March 12, 2012


                                   MADIWANI CHADEMA WAMLIPUA MAGUFULI



                                         Waziri wa Ujenzi John Magufuli

Na Daniel Limbe,Chato
MADIWANI wa halmashauri ya chato mkoani kagera kupitia tiketi ya Chadema wamemlipua mbunge wa jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli kwa madai amekuwa akitoa lugha za uchochezi na kejeli kwenye mikutano yake ya hadhara pindi anapokuwa akizungumza na wananchi kwenye kata za madiwani wa upinzani.

Akitoa kauli hiyo leo (jana) kwenye kikao cha baraza hilo,diwani wa kata ya Muganza Marko Maduka amedai mbunge wa jimbo hilo amekuwa akitumia lugha chafu kwa wananchi, huku akitamka hadharani kuwa serikali haitopeleka maendeleo kwa wananchi hao kwa madai ya kuwachagua viongozi wa upinzani ndani ya jimbo lake.

Hatua hiyo imefuatia swali la papo kwa papo lililoulizwa na diwani wa kata ya Nyamirembe John Ibawa kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Chato Charles Maisha ambaye alitaka kujua kanuni zinazowaruhusu madiwani wa upinzani kufanya mikutano ya hadhara kwenye kata za madiwani wa CCM na kuwachonganisha kwa wapiga kura wao.

Swali hilo lilionekana kuchafua hali ya hewa kwenye baraza hilo,baada ya kumtuhumu vikali diwani wa kata ya Buseresere Crespen Kagoma kwa madai amekuwa akilenga kuchochea vulugu kwa wananchi dhidi ya madiwani wa chama tawala.

Hatua hiyo ililazimu madiwani wa Chadema kumhusisha mbunge wa jimbo hilo kutokana na kauli zake chafu na kejeli kubwa kwa wananchi wanaoongozwa na madiwani wa upinzani, na kuwataka madiwani na viongozi wa CCM kumshauri mbunge huyo kuacha kutoa kauli za uchochezi kwenye kata zao ili kudumisha demokrasia katika wilaya hiyo.

“Mheshimiwa mwenyekiti mimi nachelea kuunga mkono kauli ya diwani mwenzangu wa CCM kwa madai madiwani wa chadema wamekuwa wakilenga kuchochea vurugu kwa wananchi wa kata za madiwani wa chama tawala...kauli za uchochezi mbona zimekuwa zikitolewa na mbunge wetu John Magufuli pindi anapokuwa kwenye kata zetu za upinzani?”alihoji diwani wa kata ya Ilyamchele Josephat Mayunga.

“Inasikitisha sana kuona madiwani wa CCM mmeshindwa kumshauri mbunge wa chama chenu…leo kauli za madiwani wa upinzani ndiyo mmeziona mbaya kuliko za Magufuli?..inashangaza kuona hajapata watu wa kumshauri”.

Akitoa mfano wa kauli za Magufuli alizozungumza na wananchi wa kata ya Muganza diwani wa kata hiyo alisema “akiwa kwangu Magufuli alisema kwa sababu ninyi mlijifanya kumchagua Chadema, Maduka kuwa diwani wenu basi kaeni namaduka wenu ili awafungulie maduka mengi..lakini ninawaahidi suala la umeme kufika Kasenda msitegemee hata kidogo”alisema

Kufuatia hali hiyo diwani viti maalumu kata ya Chato Brandina Mwarabu (CCM) aliwasihi madiwani wenzake kuacha kuogopa kusemwa na wapinzani badala yake amewataka pale wanaona wamezungumzwa hawana budi nao kuitisha mikutano na kuzungumza na wanachi ikiwezekana kukanusha kauli hizo badala ya hoja hizo kuzipeleka kwenye baraza la madiwani.

Jitihada za kumpata Mbunge wa jimbo la Chato Magufuli hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkoni kutopatikana.

                                                        

Thursday, March 8, 2012




Daniel Limbe,Reporter Chato
Day after new teachers over 60 secondary school district Geita Mwanza sleep at the office of director of the council the press paid deserving their other teachers 50 in the councils of Chato region have rolled out at the office of the council of their demanding monthly salaries, fares and subsistence allowances.

Speaking to this newspaper today some of those teachers who however did not like their names written newspaper have said they have failed to afford the cost of living on stations work after due to lack of funds to enable them to survive a situation that has led some female teachers to engage in sexual relations in order to afford life.

The police district here limeimalisha protection in the area for more than 2 hours until they were leaving teachers to avoid possible extinction for breach of peace.


Likewise asked to describe the amount assumed by those teachers director, he has claimed not to have accurate data and that might be available should be given enough time to claim today he had the ceremony on the women around which the district level have been made to the village and county Katende.

Acting director of the District Ishengoma Kyaruzi has claimed that the demands of the teachers they are correct, except they have to pull the patient while the council continues to make contacts and do not have the money and that he had given "the website" the ministry so that when they found the money given to go and carry on the District.

Their claims are the wages of February, remittances for 4 days after they had paid 3 days the amount of Tsh 135,000 instead of 7 days and money to transport their luggage, money that have been beaten chip indeed hour by hour with the director Hamida Kwikwega failing when they wanted to know sure of their money.

The move that led police to the area of ​​the council of Chato and scatter these teachers claimed focuses disappointing in demanding their rights from the assigned amount of Shs 135,000 to sustain for more than 40 days as they promised their claims for days that have no implementation.

Tuesday, March 6, 2012


.WALIMU GEITA WAKESHA OFISI YA MKURUGENZI WAKISHINIKIZA KULIPWA MADAI YAO
. WADAI WAPO TAYARI KUFA KWA KUDAI HAKI YAO
. DED ASUSIA KIKAO BAADA YA HOJA ZAKE KUPINGWA VIKALI


             Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa.

Na Daniel Limbe,Geita
KATIKA hali inayoonekana kuiumiza kichwa serikali kutokana na migomo na maandamano ya watumishi kila kukicha, hali hiyo imezua tafrani wilayani Geita mkoani hapa baada ya walimu wapya zaidi ya 60 wa shule za sekondari kuandamana hadi ofisi za mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mpangalukera Tatala wakidai kulipwa stahiki zao ambazo wamedai kupigwa danadana kila uchwao.

Hatua hiyo iliwalazimu siku ya jana kukesha usiku na mchana mbele ya ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kuiusia serikali kuacha kuwanyanyasa kutokana na madai yao huku shughuli mbalimbali za kiofisi zikiwa zimesimama kwa muda usiojulikana kutokana na kuhofia usalama wa watumishi.

Baadhi ya nyimbo walizokuwa wakiimnba ni pamoja na ule wa “kama siyo juhudi zako nyerere uongozi wangepata wapi!!...na ule wa tunataka haki zetu..”

Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo na ofisa elimu sekondari wa Wilayani hiyo walilazimika kukutana na walimu hao kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo ili kuzungumza nao na juhudi hizo kugonga mwamba baada ya walimu hao kupinga kila alichokuwa akizungumza mkurugenzi huyo ambaye alichukia na kuwaacha ukumbini.

Ofisa elimu ya sekondari wilayani Geita, George Opiyo, alilieleza gazeti hili kuwa walimu hao walivamia eneo hilo tangu machi 4 mwaka huu majira ya asubuhi, wakiimba  nyimbo mbalimbali za mapambio ambapo mbali na uongozi wa halmashauri hiyo kukutana nao kuwaeleza hali halisi bado walimu hao wamegoma kurudi kwenye vituo vyao vya kazi hadi hapo watakapolipwa madai yao.

Opiyo alisema walimu hao wanadai mishahara yao ya mwezi mmoja tangu waanze kazi Februari mwaka huu, fedha za kujikimu za siku 7,walimu wa shahada siku 3 na stashahada 4 na nauli ya kusafirisha mizigo yao kwenda vituo vya kazi,na kwamba wanadai jumla ya Tsh. Mil 40,037,100 za awamu ya pili baada ya pesa za awamu ya kwanza Tsh. 30,150,000 kati ya Tsh. Mil 70,187,100 walizokuwa wanadai walikwishawalipa.

Kwa upande wake katibu wa Chama cha Walimu Wilayani Geita Samwel Hewa mbali na kukutana na walimu hao leo,amelaani vikali unyanyasaji huo na kuiomba serikali iwarudishe nyumbani walimu hao hadi hapo itakapopata fedha za kuwalipa na siyo kuwatesa kama inavyofanya sasa hali iliyopelekea walimu hao kulala bila kula nje ya ofisi za halmashauri hiyo kama wanyama.
                                                                   











Saturday, March 3, 2012

                                     SERIKALI YAKIRI KUWABAMBIKIZA KESI WANANCHI

Katibu tawala wa wilaya ya Biharamulo  Masoud Biteyimanga akijibu baadhi ya hoja katika mjadala wa elimu ya katiba uliofanyika wilayani humo hivi karibuni PICHA na Daniel Limbe

Na Daniel Limbe,Biharamulo
HATIMAYE serikali imekiri hadharani kuwabambikiza kesi baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa dini kisha kuwatupa gerezani kutokana na madai ya kuvunja sheria za nchi kwa makusudi huku wakijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria kauli ambayo inadaiwa kumkera Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Dk Antony Mbasa na kuamua kususia chakula.
   
Hatua hiyo imeatofasiliwa na baadhi ya wananchi kuwa ni kulinda maslahi serikali ambayo kama si kufanya hivyo maendeleo yaliyopo yasingeliweza kufikiwa na kwamba ili maendeleo ya kweli yapatikane lazima baadhi ya watu waumie kwa ajili ya wengine.
Akizungumza na baadhi ya wananchi,viongozi wa vyama vya siasa,madhehebu ya dini na taasisi mbalimbali za serikali na kiraia waliohudhulia kwenye mjadala wa elimu ya katiba  wilayani Biharamulo mkoani kagera iliyotolewa na mtandao wa mashirika ya siyo ya kiserikali mkoani humo (Kangonet), katibu tawala wa wilaya hiyo (DAS) Masoud Biteyimanga alikiri serikali kuwabambikiza kesi baadhi ya wananchi na viongozi wa madhehebu ya dini wilayani kwake
.
Kauli hiyo ambayo haijawahi kutolewa na kiongozi yeyote wa serikali hapa nchini,imekuja huku baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakilalamikia vyombo vya dola kuwabambikizia kesi kinyume cha sheria kwa maagizo ya wakubwa wao kutoka serikalini.

Biteyimanga alikuwa amemwakilisha mkuu wa Wilaya hiyo ya Biharamulo Ernest Kahindi kwenye mjadala wa utoaji elimu ya katiba iliyokuwa ikitolewa na mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kagera na yale ya wilaya ya Biharamulo (Bingonet) ambayo yalifanyika katika ukumbi wa shule ya msingi biharamulo kwa ufadhili wa shirika la The Foundationi for Civil Society.

Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu ushauri na mapendekezo ya mchungaji Cosmas Lugemalila wa kanisa United Pentecoste Church (UPC) lililopo wilayani humo aliyetaka kujua iwapo serikali inao mpango wa kuingiza kwenye katiba mpya kipengele cha kuwabana watu,wakiwemo viongozi wa umma ambao wamekuwa wakiwadhihaki wao pamoja na madhehebu yao hali inayoonysha wazi kuwa viongozi wa dini kutelekezwa na serikali.
 
Akizungumza kwa kujiamini na bila kutafuna maneno,mbele ya mbunge wa jimbo hilo,viongozi wa asasi za kiraia,na wananchi mbalimbali waliokuwemo ukumbini hapo huku akiyakejeli madhehebu ya dini za kikristo Biteyamanga alisema,"Hii nchi ni ya amani na utulivu...inaongozwa kwa misingi ya sheria ambazo zimeainishwa kwenye katiba unaposema viongozi wa dini hawashirikishwi na wamekuwa wakitengwa na kudhihakiwa si kweli"

Akitoa mfano hai ili kuthibitisha madai hayo ya serikali kushiriki kuwabambikizia kesi wahusika ili isionekane anazungumza maneno ya uongo alisema,"Tumewahi kumkamata mchungaji mmoja huko Katahoka...huyo mchungaji kazi yake ilikuwa ni kustarehe nyumbani kwake huku akiwazuia wananchi kuchangia maendeleo...tulimkamata na kumuundia ajali (kumbambikizia kesi) na tuliopomtupa gerezani kwa sasa ametoka huko akiwa amenyooka kabisa"alisema


Hata hivyo katika kile kilichodaiwa ni kukerwa na kauli ya kiongozi huyo wa umma anayewakilisha serikali ngazi ya wilaya,Mbunge wa jimbo hilo Dk Mbasa (Chadema) hakuweza kushiriki chakula,na hata alipoulizwa sababu alikanusha madai hayo nakudai alikuwa akiwahi wapiga kura wake aliokuwa amewaacha nyumbani kwake.

                                                                     

Friday, March 2, 2012

MKUU WA MKOA  ADAIWA KUKWAMISHA UCHUMI KAGERA






BAADHI ya wananchi wa wilaya za mkoa wa kagera wamedai kukerwa na agizo la mkuu wa mkoa huo Kanal Mstaafu Phabiani Masawe kuwataka kusitisha shughuli zao za kiuchumi kwa saa 4 kila alhamisi ya wiki kwa lengo la kufanya usafi wa mazingira mkoani humo


Hatua hiyo imedaiwa kuwa kikwazo kikubwa cha uchumi kwa wananchi kutokana na muda huo kushindwa kuzalisha mali na kulazimika kujikita katika usafi wa mazingira mbali na kwamba shughuli za usafi hufanyika kila siku kwenye majumba yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wananchi hao ambao hawakuwa tayali kuandikwa majina yao, kutoka wilaya za Bukoba,Muleba,Misenyi Karagwe, Ngara,Biharamulo na Chato wameonyesha wasiwasi wao mkubwa katika kupunguza hali ya umaskini mkubwa uliopo hivi sasa iwapo serikali itaendelea na msimamo huo.

Aidha wamedai kukerwa na hatua ya kuzuiwa kufunguliwa kwa maduka ya madawa,Migahawa na huduma za usafiri mpaka kukamilika muda wa kufanya usafi, hatua mabayo inaweza kuongeza madhara makubwa kwa binadamu ikiwa ni pamoja na vifo baada ya wagonjwa kukosa dawa walizoamliwa kununua kwenye maduka hayo.

Hata hivyo wameiomba serikali kuwatumia viongozi wa vitongoji na vijiji katika kukagua usafi kwa kila kaya badala ya kuwataka wananchi kusitisha shughuli zao kwa saa nne pasipo kuzalisha mali ili hali inayoweza kuchangia ongezeko kubwa la umaskini wa vipato.

Jitihada za kumpata mkuu wa mkoa wa kagera Masawe hazikuzaa matunda baada simu zake za mkononi kutopatikana wakati wote alipopigiwa.






KULEMAA VIUNGO SIYO SABABU YA KUWA MASKINI

 Mmoja wa walemavu wa viungo wa kikundi cha Budap cha mjini Bukoba Bw, Elias Zacharia akiwa katika moja ya majukumu yake ya kila siku akiandaa ngozi kwaajili ya kutengeneza ngoma.

Baadhi ya wavuvi katika ufukwe wa ziwa victoria ukanda wa Bukoba mkoani kagera wakiandaa nyavu zao kwaajili ya kwenda kuvua samaki.PICHA na Daniel Limbe

Wanahabari wa chama cha waandishi mkoani kagera (KPC) wakipata maelekezo juu ya uendeshaji wa kituo cha kusafirisha watalii mkoani humo (KIROYERA). PICHA na Daniel Limbe.


Moja ya gengo la Kampuni ya kusafirisha watalii mkoani kagera ambalo baadhi ya waandishi wa habari  mkoani humo walikwenda kupata maelekezo juu ya shughuli za kitalii zinazofanyika hapo.

Mmoja wa walemavu wa kikundi cha BUDAP Elias Zacharia akiwa katika shughuli za uandaaji wa ngoma.


 Baadhi ya zana za kitalii zilizotengenezwa na walemavu wa kikundi cha Budap zikiwa tayali zimeshaandaliwa kwaajili ya kuuzwa kwa wananchi wa ndani na nje ya nchi.