Tuesday, December 11, 2012


           KAMA HALI NDIYO HII ULINZI WA RAIA NA MALI ZAO UPO MASHAKANI.

Askari wa kituo kidogo cha polisi cha Buziku wilayani chato mkoani geita wakiwa wameuchapa usingizi majira ya saa 7:30 mchana kama walivyokutwa na mmiliki wa blog hii.

Friday, December 7, 2012


                                        VITAMU LAKINI VINAMADHARA YAKE


Wednesday, December 5, 2012

BAADHI YA VIKOMBE VILIVYOTOLEWA KWENYE MASHINDANO YA TAMASHA LA JIFUNZE BILA UOGA WILAYANI GEITA.....YALIYOANDALIWA NA MASHARIKA YASIYO YA KISERIKALI WILAYANI GEITA YA PLAN INTERNATIONAL NA THE INFORMED RURAL SOCIETY.

     VIONGOZI WAPYA WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU MKOA WA GEITA (GEREFA)


Sunday, December 2, 2012

BAADHI YA MATUKIO KATIKA ARUSI YA BW,SAMIR SHIDA LUDOMYA NA        BI,MARIAM MKUMBO SHEREHE AMBAZO ZILIFANYIA CHATO KATIKA UKUMBI WA GIRAFFE PUB.


PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA MKUU WA POLISI NCHINI SAID MWEMA ALIPOTEMBELEA WILAYANI CHATO MKOANI GEITA.
















Tuesday, November 27, 2012



WATOTO SABA WANUSURIKA KUFA CHATO.



                       Waziri wa ujenzi Dk John Mafufuli akitoa maagizo ya kukamatwa mhudumu wa afya.

Na Daniel Limbe,Chato
WATOTO Saba wamenusurika kuawa kwenye hospitali ya wilaya ya Chato mkoani geita baada ya mhudumu wa afya Maliagoreth Kyaruzi kuwanyofolea maji yenye dawa (drip) wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya watoto kwa madai ya ndugu zao kukataa kufanya usafi wa vyoo vya hospitali hiyo.
 
Watoto walionusurika na vifo hivyo ni Edward Robert(4)mkazi wa kijiji cha Nyamirembe,Kashinje Lukanya(12) mkazi wa Busaka,Iren Nasib(3)mkazi wa Bwanga,Naomi Tumain(5) mkazi wa Kachwamba,Yunis William(3)mkazi wa Kasala,Astelia Siajali(2)mkazi wa Kahumo na Alphonce Makolobelo.
 
Tukio hilo la kusikitisha limetokea leo majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya mhudumu huyo wa afya kuwataka ndugu za wagonjwa wote walilazwa kwenye wodi ya wanawake na watoto kwenda kufanya usafi wa vyoo kutokana na kuwepo kwa uchufu unaodaiwa kusababishwa na wagonjwa wenyewe.
 
Wakizungumza na Blog hii baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo William Masai na Ester Misungwi wamesema hatua hiyo ilikuja baada ya ndugu za wagonjwa kukaidi amri iliyotolewa na mhudumu huyo aliyewataka kuondoka ndani ya wodi hizo na kwenda kufanya usafi kwenye vyoo vya hospitali hiyo.
 
Baada ya wananchi hao kukaidi amri hiyo mhudumu huyo anadaiwa alilaejea na kuanza kunyofoa maji yenye dawa yaliyokuwa yamening’iniziwa kwa wagonjwa kwaajili ya matibabu kisha kuondoka ndani ya wodi hiyo huku akiwataka watu walioumizwa na kitendo hicho kushitaki popote watakapo ona panafaa.
 
Hatua hiyo iliwalazimu baadhi ya ndugu za wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kuutafuta uongozi wa haospitali hiyo kabla ya kuwasiliana na katibu wa mbunge wa jimbo la Chato Gelvas Stephano ambaye naye alizungumza na waziri wa ujenzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo ambaye alifika eneo la tukio akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
 
Kufuatia hali hiyo Waziri Magufuli alilazimika kuzungumza na wagonjwa,na watumishi wa afya kwa lengo la kusikiliza kero zao muda mchache baada ya kumaliza kujionea hali halisi ya watoto waliokuwa wamenyofolewa drip za dawa kisha kulejeshwa baada ya ndugu za wagonjwa kulalamika.
 
Kutokana na malalamiko mengi yaliyotolewa na wagonjwa kuhusu vitendo vinavyofanywa na mhudumu huyo Waziri Magufuli amelazimika kumwagiza mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kuhakikisha wanamtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
 
“Bahati nzuri mkuu wa wilaya upo hapa,na Ocd na wewe upo hapa…ninaagiza huyo Maliagoreth akamatwe mara moja na kesho afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za kutaka kuuwa wagonjwa saba kwa makusudi”alisema Magufuli
 
“Nasema huyo siyo mhudumu anayetakiwa kufanya kazi ya afya…maana kuwanyofolea drip wagonjwa kwa kosa la ndugu zao kukataa kufanya usafi wa vyoo haliwezi kufumbiwa macho….huyo maliagoreth hafai na ninaomba kuanzia leo asikanyage hapa kwenye hospitali kuja kuhudumia wagonjwa…maana ipo siku hata mimi ataninyofolea drip,naamini mmenielewa”alisema Magufuli na kushangiliwa na wagonjwa.
 
Kadhalika magufuli aliwataka waganga na wauguzi wengine kutoa huduma nzuri kadri ya inavyopaswa na kuwatahadhalisha iwapo watawahudumia wagonjwa vibaya kwa lengo la kulipiza kisasi kwa madai wagonjwa wamewashitaki kwake ambapo amedai kufanya hivyo itakuwa ni kutowatendea haki wagonjwa.
 
Vilevile amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Shaban Ntarambe kuhakikisha anamsimamisha kazi mara moja nesi huyo kwa madai hana sifa za kuendelea kuwa mtumishi kwenye wilaya ya chato.
 
Mkuu wa wilaya ya chato Rodrick Mpogolo mbali na kudai kusikitishwa na tukio hilo ameahidi kuunda tume maalumu itakayochunguza utolewaji wa huduma za afya kwa wananchi wanaofika kutibiwa hapo kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi.
 
Aidha amesema msingi wa serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora na kwamba dosari zinazojitokeza atahakikisha zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu ili kusijitokeza vitendo kama vilivyojitokeza.
 
Kwa upande wake Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Dk Pius Buchukundi amekiri  kutokea tukio hilo na kudai kuwa kitendo kilichofanywa na mhudumu wake siyo msimamo wa hospitali bali ni matakwa yake mwenyewe na kwamba atahukumiwa kwa matendo aliyoyatenda yeye mwenyewe.
 
Dk Buchukundi amewataka wagonjwa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa hospitali hiyo ili kila kunapojitokeza mapungufu kama hayo yaweze kushughulikiwa haraka badala ya kukaa kimya na kuondoka wakinung’unika.
 
 
 
 

Monday, November 26, 2012


                                             JWTZ LATOA UFAFANUZI MLIPUKO NGARA.


Na Daniel Limbe,Ngara
JESHI la wananchi wa Tanzania  JWTZ  kikosi cha Faru makao makuu ya  Tabora limetoa ufafanuzi juu ya msihndo mkubwa uliojitokeza wilayani ngara mkoani kagera na kusababisha baadhi ya wananchi kuyakimbia kwa muda makazi yao kwa kuhofia maisha kutokana na kile walichodai bomu lilidondoka kwenye kijiji cha Ruganzo wilayani humo.

Katika tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa Novemba 22 majira ya saa nane lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya ya ngara kuishi kwa hofu kubwa kutokana kitu kisichofahamika kudondoka toka angani na kusababisha mshindo mkubwa mithili ya tetemeko la ardhi hali iliyopelekea baadhi ya nyumba kupata nyufa.

Kufuatia hali hiyo kiongozi wa kikosi cha JWTZ  Mnadhimu mkuu wa mafunzo  na utendaji wa kivita Brigedia ya Faru Kanali Simon Lali Hongoa amelazimika kutoa ufafanuzi wa kitu hicho baada ya wataalamu wa mabomu kufika kijiji cha Ruganzo kata ya Kibimba wilayani Ngara na kufanya uchunguzi wa kina baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kushindwa kubaini ni kitu gani pamoja na madhara yake.
Kanali Hongoa alikanusha vikali madai ya wananchi wa ngara kuwa kitu kilichodondoka wilayani humo kilikuwa ni bomu la kivita na kudai kuwa maneno hayo hayakuwa na ukweli wowote kwa kuwa kilichodondoka kilikuwa ni kipande cha setelaiti iliyokuwa ikisafiri angani na inahofiwa kiliishiwa nguvu na kudodoka  katika eneo hilo.

Aidha alidai kuwa uchunguzi wa kitaalamu umebainisha kuwa setelaiti hiyo haina madhara yoyote na wala haikutoka uelekeo wa nchi jirani zinazoendelea na migogoro ya kivita kama baadhi ya maelezo ya wananchi wa wilaya hiyo walivyodai.
Hangoa alisema pamoja na kutokuwepo madhara kila mwananchi anatakiwa kuchukua tahadhari ya kubeba vitu wasivyokuwa na uhakika navyo wakilenga kutaka kupata utajiri wa haraka ambao unaweza kuhatarisha maisha yao na jamii inayowazungukana sanjari na kuleta matatizo kwa taifa.
“Kila inapotokea mtu yeyote akaona kitu ambacho hana uhakika nacho usikichukue kwa masuala ya kupata dili utakuja kufa na kuua familia  ni bora ukatoa taarifa katika vyombo vya usalama”.Alisema Hongoa
 Alitoa mfano wa baadhi ya matukio kama hayo yaliyotokea hivi karibuni ambayo yalisababisha madhara makubwa kwa watoto  wilayani karagwe na Arusha na kusababisha  hasara kwa wazazi wao na hata taifa kwa kupoteza rasilimali watu ambao wangekuwa wazalishaji wa uchumi wa taifa.
Awali kabla  kikosi hicho kutoka Tabora hakijawasili wilayani Ngara kulifika kikosi  cha wataalamu wa kambi ya JWTZ Biharamulo lakini uchunguzi wao ulitia mashaka na kulazimika kutoa taarifa ngazi nyingine kwa ajili ya uchunguzi wa kina licha ya baadhi ya wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya kibimba kuonyesha utukutu wao kwa kukinyanyua kutoka kilikotua na kukipeleka jirani zaidi na  shule yao zaidi ya mita 500
Kitu hicho kizito kilidondoka usiku wa manane na kuzama nusu yake ardhini kwa ukubwa wa diameta 50 kilomita mbili nje ya uwanja wa ndege wa kijiji cha  Ruganzo ambapo baadhi ya raia  walidhani kuwa ni Kimondo,kilichodondoka na kusababisha mshindo mkubwa uliosikika wilaya nzima na  nchi za jirani.
Akihutubia wananchi Mwenyekiti wa kijiji cha Ruganzo  kata ya kibimba wilaya ya  Ngara mkoani Kagera Salvatori Mbanyi  alisema kuwa kitu hicho kilidondoka kutoka angani na mshindo wake kuwashtua wananchi na asubuhi yake kilionwa na watu karibu na mto Ruvubu unaopita kijiji humo kutoka mpakani mwa nchi ya Burundi kuelekea Rusumo mpakani mwa Ngara na Rwanda.
Mbanyi alisema kuwa mara baada ya wananchi kuona kilichosababisha mlipuko viongozi walipeleka taarifa kwa  jeshi la polisi pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya kupata maelekezo na ufafanuzi zaidi  ambapo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ilianza kazi yake .
Alisema kadri masaa yalivyosogea asubuhi umbo lake liliongezeka na kutanuka kama vile kinataka kulipuka na baadaye hali hiyo iliisha na  baadhi ya wananchi  walianza kukisogelea na kukigusa  kisha  kujaribu kukihamisha huku  watoto na wanafunzi wakikinyofoa nyuzi zilizokifunika                                                                         
                                            Taswira ya setelaiti iliyodondoka wilayani ngara.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu alisema kutokana na kitu hicho kuanguka eneo la wilaya yake lilisababisha taharuki kubwa kwa wananchi ambapo baadhi yao waliamini kuwa ni kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka kutokana na vita vinavyoendelea kwenye nchi ya DRC dhidi ya waasi wa 23 na majeshi la serikali.

Kamanda wa polisi mkoani kagera Philip Karangi aliwataka wananchi wa ngara kushilikiana na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kwa kutoa taarifa za kiusalama mapema ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza badala ya baadhi ya wananchi kufanya kazi za kitaalamu zisizowahusu hali inayoweza kusababisha madhara makubwa kutokana na uzembe.

Kikosi cha Brigedia ya Faru Makao makuu ya Tabora kinasimamia mikoa minane ya Kanda ya ziwa ikiwa ni Tabora,Shinyanga,Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Kagera na Kigoma.
                                                                          Mwisho.

Sunday, November 11, 2012

                             Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya geita wakiwa katika kikao cha baraza.

Na Daniel Limbe,Geita
WIKI moja baada ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani hapa kumkataa Daktari wa mifugo Thobias Kiputo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwadharau na kufunga minada ya mifugo wilayani humo kwa madai ya kuwepo ugonjwa wa miguu na midomo kwa lengo la kuikosesha halmashauri mapato,madiwani hao wameendelea kuonyesha msimamo wao na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumwondoa wilayani humo.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya geita Charles Kimaro wakati akiwasilisha taarifa ya ugawanywaji wa watumishi na mali za halmashauri ya geita kwa lengo la kuzitenganisha halmashauri tatu kiutawala kutokana na serikali kuanzisha halmashauri ya mji wa geita na halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale.
 
Baada ya Kimaro kuwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha baraza la madiweani kilichoketi leo ili kuivunja halmashauri ya geita na kuanzisha rasmi halmashauri ya mji wa geita na halmashauri za wilaya ya Nyang’hwale na Geita ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya madiwani walionyesha kutaharuki kutokana na kuendelea kulisikia jina la Dk Kiputo.
 
Akichangia hoja ya ugawanaji wa watumishi,mali na madeni ya halmashauri ya wilaya ya geita Diwani wa kata ya Nzera Joseph Musukuma alisema kitendo cha kuendelea kusikia jina la Daktari huyo ndani ya orodha ya watumishi wa halmashauri ni kutowatendea haki kwa kuwa tayari walikwisha azimia kuondolewa kwa mtumishi huyo ndani ya wilaya ya geita.
 
“Mheshimiwa mwenyekiti ninasikitika sana kuendelea kumsikia huyo daktari akiwa kwenye idadi ya watumishi wa halmashauri yetu…tulisha mkataa na kamwe hatumtaki kwenye wilaya yetu…kama ni taratibu za kisheria zifanyike lakini akiwa nje ya wilaya hii… kama hakuna pakumpeleka mrudisheni alikotoka kabla ya kuja wilayani kwetu”alisema Musukuma kwa jazba kali.
 
Kauli hiyo ilisababisha takribani madiwani watatu kuchangia hoja hiyo huku wote wakionyesha msisitizo kuondolewa kabisa jina Daktari huyo huku wakidai kuendelea kulisikia jina hilo nikuwadhihaki madiwani hao kwa kuwa tayari walisha mkabidhi jukumu la kumfukuza kwenye halmashauri yao .
 
Kutokana na hali hiyo gazeti hili lililazimika kumtafuta Daktari huyo amnbapo alipuuza uamuzi huo na kulazimika kuelezea sababu za baadhi ya madiwani hao kumkataa kuendela kufanya kazi kwenye halmashauri hiyo kutokana na alichokisema kuwa baadhi yao wanamiliki zabuni za kukusanya ushuru kwenye minada aliyoifunga kisheria baada ya kuwepo ugonjwa wa miguu na midomo.
 
Aidha alifafanua kuwa pamoja na kumtuhumu kwa sababu mbalimbali baadhi ya madiwani hao wanamiliki maduka ya kuuza pembejeo za kilimo na mifugo licha ya kuwa hawana utalaamu wa kutoa huduma hiyo mhimu hali ambayo imeonekana kuwapunguzia mapato.

“Lakini suala la kufunga minada ya mifugo ni la kitaalamu zaidi…na taratibu za kufunga minada hiyo ilizingatia sheria taratibu na kanuni…na ifahamike kuwa hayo hayakuwa maamuzi yangu binafsi isipokuwa ni agizo la wizara husika ambayo iliazimia kuwekwa karantini ya kuchanja mifugo wote waliopo geita ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo usilete madhara kwa binadamu.
 
Hivi karibuni ikiwani Novemba 1 mwaka huu baraza la madiwani wa halmashauri hiyo liliazimia kuondolewa kwa daktari huyo kwa madai ya utendaji kazi wake kutokuwa na kulidhisha,kujibu jeuri kwa viongozi wenzake pamoja na madiwani hao huku wakimtuhumu kumiliki kampuni ya kutoa chanjo ya mifugo kwa maslahi yake binafsi.
                                                  ELIMU YA AWALI CHATO INATIA AIBU.

Baadhi ya watoto wa shule ya awali katika shule ya msingi Kalema wakiwa wanaendelea na masomo kama walivyokutwa na mmiliki wa blog hii.

Sunday, October 28, 2012


                      WANANCHI  GEITA WAKIFUATILIA HABARI KATIKA MAGAZETI

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya geita mkoani geita wakifuatilia habari mbalimbali katika magazeti kama walivyokutwa na mmiliki wa blog hii.Picha Daniel Limbe.

Saturday, October 27, 2012

                           WALIMU SENGEREMA WATWANGANA MAKONDE OFISINI.

Na Daniel Limbe,Sengerema
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida,walimu wawili wa shule ya msingi Igaka wilayani Sengerema mkoani mwanza wametwangana makonde ndani ya ofisi ya shule baada ya kurushiana maneno makali kutokana na mwalimu mkuu msaidizi kumtuhumu mwenzake kwa uwajibikaji mbovu.

Akizungumza na NIPASHE mwalimu mkuu wa shule hiyo Boniphace Shilunga amesema tukio hilo limetokea juzi oktoba 19 mwaka huu majira ya saa 8 mchana baada ya mwalimu Lazimani Manyabele kusukumiana makonde na mwalimu mkuu msaidizi Edson Kagusa.

Hatua hiyo ilitokana na majibizano ya maneno kati ya walimu hao wawili baada ya mwalimu mkuu msaidizi kumtuhumu mwenzake kuwa ni amekuwa akivunja sheria za kwa makusudi kutokana na kuchelewa kufika shuleni na kushindwa kuhudhuria kwenye vipindi kama alivyopangiwa.

Amesema baada ya kurushiana maneno ndani ya ofisi hiyo mwalimu Manyabele alinyanyuka mahari alipokuwa ameketi na kumkwida mwalimu mwenzake baada ya kumwita kuwa msaliti hatua iliyosababisha kumrushia konde lililopelekea majibizano ya ngumi hizo kabla ya walimu wengine kuingilia na kuwaachanisha.

Amedai kuwa mbali na sheria za nchi zinazowataka watumishi kuwahi kazini na kutimiza wajibu wao,shule hiyo tayari ilikuwa imejiwekea utaratibu wa walimu wote kufika shuleni kabla ya saa 2 asubuhi sanjari na kuhudhuria kwenye vipindi vyote vya masomo ikilinganishwa na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakifika shuleni saa 4 asubuhi na kuondoka pasipo utaratibu unaotakiwa.

Mratibu elimu kata ya Buzilasoga Robert Cheyo amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa tayari amekwisha andaa taarifa ya maandishi kwenda kwa ofisa elimu wa wilaya hiyo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya walimu hao kwa madai kupigana maeneo ya shule ni kuidhalilisha shule na taaluma ya ualimu.
Amesema kamwe serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo kwa kuwa ni utovu wa nidhamu kazini na uzalilishaji wa taaluma ya ualimu kwa kuwa wao wanatakiwa kuwa kioo kwa jamii wanayoiongoza.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya sengerema Juma Mwanjombe aliupoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na tukio hilo alidai kuwa tayari ofisi yake imekwisha pokea taarifa ya sakata hilo huku akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria walimu hao ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kama hiyo.

Mwanjombe alifafanua kuwa walimu hao wamevunja sheria namba 56 ya mwaka 2003 ambayo inawataka walimu kuwa na mahusiano bora kazini na kwamba inabainisha wazi kuwa atakaye vunja sheria hiyo adhabu yake ni kupewa onyo kali,kutelemshwa daraja la kazi,au kufukuzwa kazi.

Aidha ametoa wito kwa walimu wote wilayani humo kutii sheria na kuheshimiana kwa kuwa ndiyo silaha ya mahusiano kazini na kwamba serikali haitamwonea aibu mwalimu yoyote atakaye endelea kuvunja sheria zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba.
    DIWANI WA NGEREJA AGEUKA OMBAOMBA,APORWA GEST NGUO,SIMU NA FEDHA

Na Daniel Limbe,Sengerema
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida diwani wa kata ya Kasenyi wilayani sengerema mkoani mwanza Sindano Sanyiwa amegeuka omba omba baada ya watu wanaosadikiwa vibaka kumpora nguo,simu ya mkononi na fedha zote alizokuwa nazo.
Sakata hilo limemkumba jana majira ya saa 8 usiku akiwa amelala kwenye chumba namba 105 kwenye nyumba ya kulala wageni ya Nyakaduha Motel iliyopo nje kidogo ya mji wa sengerema wakati akihudhulia vikao vya baraza lahalmashauri hiyo.
Hatua ya diwani huyo kugeuka ombaomba imekuja baada ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo Methew Lubongeja kumpa nafasi ya kuuliza swali kwenye kikao cha baraza la madiwani,ambapo diwani huyo kabla ya kuuliza swali aliomba kulijulisha baraza hilo kuwa ameibiwa nguo zake,simu ya mkononi na fedha zilizokuwa kwenye mfuko wa suluali yake.
Kutokana na hali hiyo aliwaomba madiwani wenzake kufanya harambee ili kumsaidia kupata kiasi cha fedha zitakazomwezesha kuendelea kumudu gharama za maisha wakati akiendelea na vikao vya baraza hilo hatua iliyopelekea madiwani hao kubwaga vicheko vingi kabla ya mwenyekiti wao kuwatuliza.
“Mheshimiwa mwenyekiti kwanza kabisa napenda kulijulisha baraza lako tukufu kuwa usiku wa kuamkia leo nikiwa nimelala kwenye chumba changu kuna watu wanaohisiwa kuwa ni vibaka walikata nyavu za dirisha la chumba hicho kisha kuniibia nguo zangu,simu ya mkononi na pesa taslimu nilizokuwa nazo,hivyo ninaomba madiwani wenzangu mnichangie changie kiasi chochote ili nami niendelee kushiriki na ninyi kwenye vikao vyetu”alisema Diwani huyo.
Hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo alifanikiwa kutuliza vicheko vilivyoambatana na makofi ndani ya ukumbi huo na kuwataka madiwani kumpa pole mwenzao kwa tukio hilo kwa kuwa linaweza kumtokea mtu yeyote pasipo kujali ni kiongozi.
Baada ya hatua hiyo diwani huyo aliendeliendelea na swali lake la msingi juu ya ujenzi wa barabara ya Kafundile kwenda kasenyi Rugongo yenye urefu wa kilomita 17 na daraja la Shitwego linaloungaisha vijiji vya Kasenyi na Rugongo ambalo limekatika na kuwafanya wakulima wa maeneo hayo kushindwa kusafirisha mazao yao kwenda kwenye soko kuu la mjini sengerema.
Vilevile alidai kuwa kutokana na hali hiyo baadhi ya wakulima,mama wajawazito na wazee wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwaajili ya kufika kwenye soko kuu,hospitali ya wilaya na huduma zingine mhimu za kibinadamu zinazopatikana mjini sengerema.
Alidai kuwa licha ya barabara na daraja hilo kutangazwa na halmashauri hiyo kwaajili ya kumpata mkandarasi hakuna hatua zozote zilizoonekana kuchukuliwa ili kunusuru maisha ya wananchi wa kata ya Kasenyi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia hali hiyo.
Kufuatia madai ya diwani huyo kuporwa mali zake NIPASHE limelazimika kufika kwenye Motel hiyo ili kupata ufafanuzi wa tukio hilo ambapo mbali na kukiri kuwepo kwa tukio hilo Meneja wa Motel hiyo Tindos Pangani amesema hatua hiyo imetokana na uzembe wa diwani huyo kwa kile alichodai alifungua dirisha na kuliacha wazi wakati akitaka kulala usiku.
“Tukio hilo lipo limetokea majira ya saa 8 usiku,lakini ninachoweza kusema ni kuwa diwani mwenyewe ndiye mzembe kwa maana wakati amelala alifungua dirisha na kuliacha wazi baadaya kuona kuna joto kali ndani huku akiwa kafungulia feni, hali iliyosababisha vibaka kupata njia rahisi ya kujipatia fedha”alisema Pangani.
Pangani amesema tukio hilo limetokea kwa mara ya pili tangu kufunguliwa kwa Motel hiyo takribani miaka 3 iliyopita na kwamba mazungumzo ya upotevu huo dhidi ya mteja wao yamefanyika na kupata suruhu.
                   WALIMU TISA WAISHI KWENYE NYUMBA MOJA SENGEREMA. 

                    Mkuu wa wilaya ya sengerema Bi Karen Yunus.(Picha   kwa hisani ya Blog)

Na Daniel Limbe,Sengerema.
KATIKA hali inayochochea misongo ya mawazo, walimu tisa wamejikuta wakiishi katika vyumba vitatu vya nyumba moja kutokana na uhaba wa nyumba.

Kufuatia hali hiyo, Baraza la Madiwani la Sengerema mkoani Mwanza limemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwatafutia nyumba mara moja walimu walimu hao.

Walimu wanaodaiwa kuishi kwenye nyumba moja yenye vyumba vitatu ni wa Shule ya Msingi Soswa wilayani hapa mkoani Mwanza baada ya kuripoti eneo la kazi na kukuta uhaba mkubwa wa nyumba za walimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Bulyaheke, Bageti Ngele kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye kata yake ambapo alisema licha ya kuwepo mafanikio makubwa ya miradi, kata hiyo inakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari, akitoa mfano wa walimu tisa wa shule ya msingi Soswa kuishi kwenye nyumba moja.

Ngele alidai hatua hiyo imekuwa ikiwaathiri walimu hao kisaikolojia na kuwa vigumu kupunguza tamaa ya mwili itokanayo na tendo la ndoa licha ya mwalimu mkuu wa shule hiyo kuishi yeye na familia yake ndani ya nyumba hiyo ambayo hata hivyo haina dari.

Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,  Mathew Lubongeja alimwagiza Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Juma Mwajombe kuhakikisha walimu hao wanaondolewa kwenye nyumba hiyo haraka wakati serikali ikijipanga kuondoa tatizo hilo.

“Kutokana na unyeti wa suala hili…mkurugenzi ninakuagiza uhakikishe walimu hao wanaondoka haraka kwenye nyumba hiyo ili ibaki idadi inayokubalika kwa kuwa hali hiyo inaweza kusababisha walimu hao kuathirika kisaikolojia…hii ni hatari sana,”alisema Lubongeja.

Aidha alisema jitihada za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha shule hiyo inaongezewa majengo ya nyumba za walimu haraka kwa kutumia fedha za serikali badala ya kuendelea kusubiri michango ya wananchi katika kutekeleza miradi hiyo.

Kaimu mkurugenzi huyo aliahidi kulishughulikia haraka suala hilo kwa kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa Umma ili kuondoa adha inayowakabili walimu hao.

Alisema hatua hiyo inaweza kuathiri kiwango cha utoaji elimu kwa wanafunzi kutokana na walimu hao kuishi kwa misongo ya mawazo.

Saturday, September 1, 2012




                                MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAENDELA KUINGIA DOSARI GEITA
                                BENDERA YA TAIFA YAZUA TAFRANI CHATO.
Na Daniel Limbe,Geita
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mbio za Mwenge wa uhuru juzi ziliendelea kuingia dosari katika Mkoa mpya wa geita baada ya Waandishi wa habari pamoja na Madereva waliokuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, kujikuta katika wakati Mgumu baada ya kuzuiwa kula chakula na Ofisa usalama wa Taifa wa Wilaya hiyo Sunday Steven.
Tukio hilo liliwakera madereva waliokuwa wakiendesha magari kwenye msafara huo na kulazimika kuingia kwenye mgomo,kabla ya mgomo huo kunusuriwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu Kapteni Honest Mwanossa.
Baada ya kumaliza kula chakula katika chumba maalum katika shule ya msingi Lugunga kiongozi wa mbio za mwenge alitoka nje na kuwafuata madereva hao waliokuwa wamejikusanya katika kundi moja wakijadili kugoma kuendesha magari hayo na kuwaomba kwenda kula chakula katika chumba hicho.
Haikufahamika mara moja mtu aliyempa taarifa kiongozi huyo wa mbio za mwenge kwamba madereva hao walikuwa wamenyimwa chakula na kwamba walikuwa katika harakati za kugomea safari,ambapo katika hali isiyokuwa ya kawaida alipomaliza kunawa alikwenda moja kwa moja na kuwafuata madereva hao mahali walipokuwa na kuwaelekeza mahali pa kula chakula.
Vilevile Mwanossa aliendelea na zoezi la kuwasaka madereva wengine ambao walionekana hawako katika mazingira hayo ambapo alikuwa akimsaka mmoja baada ya mwingine na kumpeleka kwenye chumba cha chakula,na baada ya hapo safari ikaanza,hata hivyo alionekana kukerwa na hali hiyo.
Madereva hao zaidi ya 11 walikumbana na mkasa huo kwa kile kilichoelezwa  na ofisa ulasama huyo wa wilaya kwamba chakula hicho kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili ya viongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8:26 mchana katika kijiji na kata ya Lugunga  wakati madereva hao  wakiwa kwenye foleni ili kupata chakula na baadaye kuendelea na msafara hadi katika shule ya sekondari Masumbwe kuzindua klabu ya kupambana na rushwa.
Walipokumbana na mkasa huo kutoka kwa ofisa usalama wa taifa walienda kujadili kuhusu suala hilo umbali wa mita 100 kutoka kwenye moja vyumba vya madarasa lililokuwa likitumika kama chumba cha kupatia chakula cha mchana katika shule ya msingi Lugunga.
Katika majadiliano hayo madereva walikubaliana kususia kuendelea na msafara wa mbio za mwenge wa uhuru kwa kuwa hawakuwa katika orodha ya wageni waliotakiwa kupata chakula hicho,kitendo ambacho kiliwafanya baadhi yao kukaa mbali na magari yao.
Pia mkasa kama huo uliwakumba waandishi wa habari sita waliokuwa wameambatana na msafara huo kutoka mkoani na wilayani humo baada ya ofisa usalama huyo kuwazuia kupata chakula cha asubuhi kilichokuwa kimeandaliwa katika ya sekondari Isangijo kata ya ushirika ambapo kiongozi wa mbio hizo aliweka jiwe la msingi kwenye chumba cha maabara.
Ofisa huyo alitumia kauli ya kwamba wanaotakiwa kupata chakula walikuwa wageni wa kitaifa na kimkoa licha ya miongoni mwa wanahabari hao kutoka mkoani ambao walikuwa wameambata na mbio za mwenge tangu ulipoingia katika mkoa wa Geita agosti 26,mwaka huu.
Mkuu wa wilaya hiyo Husna Mwilima ambaye naye alionekana kukerwa na kitendo cha Ofisa usalama huyo,alizungumza baadaye na waandishi wa habari na kuwaomba radhi kwa yote yaliyojitokeza,na kuwataka kuendela na zeozi hilo la kukimbiza mwenge katika wilaya hiyo.
"Jamani Ndugu kila binadamu ana mapungufu yake,naomba mumsamehe alikua hajui alitendalo,namuombea msamaha wa dhati kabisa,jamani wilaya yangu ni Mpya,na naweza kuwathibitishia kwamba wilaya mama (Bukombe) imenitenga sana katika zoezi hili nimhangaika sana na huyu ofisa usalama yanwekena amechanganyikiwa....'' alisisitiza mkuu huyo wa wilaya.
Hatua hiyo ilikuja siku moja baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti habari za mkuu wa wilaya ya Geita Omary Mangochie  kupoteza mbio za mwenge wa uhuru baada ya kupitiliza mradi  mmoja uliotarajiwa kukaguliwa na kiongozi wa mbio hizo Kapten Mwanosa katika kijiji cha Nyamalimbe.
Tukio hili lilitokea baada ya kiongozi huyo kupitiliza umati mkubwa wa watu waliokuwa wamepanga foleni barabarani kusubiri kuupokea mwenge huo ili kukagua na kutoa mkopo  kwenye kikundi cha mikopo na akiba cha kijiji hicho.
Baada ya mbio hizo kukimbia umabli wa kilomita 3,kiongozi huyo alipoipitia ratiba ya mkoa aligundua kupitilizwa mradi huo huku mkuu wa wilaya akiwa amekaa kimya kitendo kilichoonekana kumkera na la kulazimika kuusimamisha msafara na kuhoji kabla ya kuamua kuendelea na msafara huo.
Mbali na hilo Mwanossa alionekana kukerwa na mapokezi ya mwenge huo katika wilaya ya chato baada ya kuufikisha mwenge wa uhuru kwenye uwanja wa mkesha na kukuta hakuna maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kutokuwepo Bendera ya taifa.
“Huu ni mwenge wa uhuru ambao tunaukimbiza kitaifa…nasikitika kufika hapa kwenye mkesha wa mwenge huu lakini sijaona bendera ya taifa ikipepea mahari hapa”alisema
Kutokana na kauli hiyo baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo ambao hawakujulikana majina yao haraka walilazimika kuwaagiza baadhi ya vijana ambao wapo kwenye mafunzo mgambo wilayani humo kwenda kung’oa bendera iliyokuwa imesimikwa kwenye ofisi za kata ya chato na kuikimbiza haraka kwenye uwanja wa mkesha wa mwenge huo.
Awali akikagua baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo Mwanossa alidai miradi mingi aliyojionea aslimia kubwa imejengwa chini ya kiwango licha ya kuwa pesa nyingi za serikali zikionekana kutumika katika miradi hiyo.
                                                                                 Mwisho.


                  MSUKUMA AOMBA KUNUSURU JAHAZI LA CCM GEITA.
                                Katibu wa itkadi na uenezi wa CCM Nape Mnauye.

Na Daniel Limbe,geita
ALIYEKUWA mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Joseph Musukuma amesema Chama cha mapinduzi mkoani humo kitafanikiwa kuzirejesha nafasi mbalimbali zilizotwaliwa na vyama vya upinzani iwapo atachaguliwa kushika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.
 
Msukuma aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa mpya wa geita ambapo alidai anakusudia kurejesha imani ya chama hicho kwa wananchi kutokana na baadhi yao kukisusia baada ya viongozi waliokuwepo awali kutokuwa na mvuto kwa wananchi.
 
Alisema CCM ni chama chenye maono mazuri kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini baadhi ya viongozi wachache wamekuwa wakikivuruga chama hicho kutokana na kutaka kujipatia maslahi binafsi kinyume cha sheria huku wananchi waliowengi wakizidi kutaabika na ugumu wa maisha. 
 
Msukuma ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nzera(CCM),alisema ameamua kuchukuwa fomu kuwania nafasi hiyo baada ya kuona wagombea wenzake wanaowania nafasi hiyo hawana sifa za kuongoza nafasi hiyo nyeti ndani ya chama cha mapinduzi.

Kufuatia hali hiyo alidai kushawishika kuomba nafasi hiyo mhimu ili kurejesha mshikamano na kukijenga chama hicho kwa kile alichodai kimepoteza sifa kutokana na baadhi ya viongozi kufanya kazi kwa mazoea na si kuwaletea maendeleo wananchi wa kipato cha chini hali ambayo imesababisha watu kukichukia na kukihama kila kukicha kwa kukimbilia kwenye vyama vingine vya upinzani.

“Nimelazimika kuchukua fomu ya uenyekiti Mkoa wa Geita baada ya kugundua wote walioomba nafasi hiyo wameshindwa kukiongoza maana wengi wao ni wale waliokuwa viongozi wa chama chetu ndani ya Wilaya na badala ya kukipeleka kwenye msitari kwa sasa kinaenda mlama hiyo ndiyo sababu kubwa ya mimi kuamua kuomba nafasi hiyo ili nikirudishe chama chetu kwenye msitari”
 
 
Kwa mjibu wa Katibu wa CCM mkoa wa geita Francis Elias tayari vigogo watatu ndani ya chama hicho akiwemo Musukuma wamechukuwa fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo wengine  ni pamoja na Daud Ntinonu aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita,na nafasi yake kuchukuliwa na mwenyekiti wa sasa John Chenge Luhemeja ambaye naye anawania kiti hicho.
 
 
Musukuma aliondolewa kwenye nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita na madiwani wenzake mapema mwaka jana baada ya kutuhumiwa kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza hadharani majina ya mafisadi wa halmashauri ya geita na kuahidi kuwaburuza mahakamani pasipo kibari cha madiwani wenzake.