JWTZ LATOA UFAFANUZI MLIPUKO NGARA.
Na Daniel Limbe,Ngara
JESHI la wananchi wa Tanzania JWTZ kikosi cha Faru makao makuu ya Tabora limetoa ufafanuzi juu ya msihndo mkubwa uliojitokeza wilayani ngara mkoani kagera na kusababisha baadhi ya wananchi kuyakimbia kwa muda makazi yao kwa kuhofia maisha kutokana na kile walichodai bomu lilidondoka kwenye kijiji cha Ruganzo wilayani humo.
Katika tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa Novemba 22 majira ya saa nane lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya ya ngara kuishi kwa hofu kubwa kutokana kitu kisichofahamika kudondoka toka angani na kusababisha mshindo mkubwa mithili ya tetemeko la ardhi hali iliyopelekea baadhi ya nyumba kupata nyufa.
Kufuatia hali hiyo kiongozi wa kikosi cha JWTZ Mnadhimu mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita Brigedia ya Faru Kanali Simon Lali Hongoa amelazimika kutoa ufafanuzi wa kitu hicho baada ya wataalamu wa mabomu kufika kijiji cha Ruganzo kata ya Kibimba wilayani Ngara na kufanya uchunguzi wa kina baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kushindwa kubaini ni kitu gani pamoja na madhara yake.

Kanali Hongoa alikanusha vikali madai ya wananchi wa ngara
kuwa kitu kilichodondoka wilayani humo kilikuwa ni bomu la kivita na kudai kuwa
maneno hayo hayakuwa na ukweli wowote kwa kuwa kilichodondoka kilikuwa ni kipande
cha setelaiti iliyokuwa ikisafiri angani na inahofiwa kiliishiwa nguvu na
kudodoka katika eneo hilo.
Aidha alidai kuwa uchunguzi wa kitaalamu umebainisha kuwa setelaiti hiyo haina madhara yoyote na wala haikutoka uelekeo wa nchi jirani zinazoendelea na migogoro ya kivita kama baadhi ya maelezo ya wananchi wa wilaya hiyo walivyodai.

Hangoa alisema pamoja na kutokuwepo madhara kila mwananchi
anatakiwa kuchukua tahadhari ya kubeba vitu wasivyokuwa na uhakika navyo
wakilenga kutaka kupata utajiri wa haraka ambao unaweza kuhatarisha maisha yao
na jamii inayowazungukana sanjari na kuleta matatizo kwa taifa.
“Kila inapotokea mtu yeyote akaona kitu ambacho hana uhakika
nacho usikichukue kwa masuala ya kupata dili utakuja kufa na kuua familia
ni bora ukatoa taarifa katika vyombo vya usalama”.Alisema Hongoa
Alitoa mfano wa baadhi ya matukio kama hayo
yaliyotokea hivi karibuni ambayo yalisababisha madhara makubwa kwa watoto
wilayani karagwe na Arusha na kusababisha hasara kwa wazazi wao na hata
taifa kwa kupoteza rasilimali watu ambao wangekuwa wazalishaji wa uchumi wa
taifa.
Awali kabla kikosi hicho kutoka Tabora hakijawasili
wilayani Ngara kulifika kikosi cha wataalamu wa kambi ya JWTZ Biharamulo
lakini uchunguzi wao ulitia mashaka na kulazimika kutoa taarifa ngazi nyingine
kwa ajili ya uchunguzi wa kina licha ya baadhi ya wananchi na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya kata ya kibimba kuonyesha utukutu wao kwa kukinyanyua
kutoka kilikotua na kukipeleka jirani zaidi na shule yao zaidi ya mita
500
Kitu hicho kizito kilidondoka usiku wa manane na kuzama nusu
yake ardhini kwa ukubwa wa diameta 50 kilomita mbili nje ya uwanja wa ndege wa
kijiji cha Ruganzo ambapo baadhi ya raia walidhani kuwa ni
Kimondo,kilichodondoka na kusababisha mshindo mkubwa uliosikika wilaya nzima na
nchi za jirani.
Akihutubia wananchi Mwenyekiti wa kijiji cha Ruganzo
kata ya kibimba wilaya ya Ngara mkoani Kagera Salvatori Mbanyi
alisema kuwa kitu hicho kilidondoka kutoka angani na mshindo wake kuwashtua
wananchi na asubuhi yake kilionwa na watu karibu na mto Ruvubu unaopita kijiji
humo kutoka mpakani mwa nchi ya Burundi kuelekea Rusumo mpakani mwa Ngara na
Rwanda.
Mbanyi alisema kuwa mara baada ya wananchi kuona
kilichosababisha mlipuko viongozi walipeleka taarifa kwa jeshi la polisi
pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya kupata maelekezo na ufafanuzi
zaidi ambapo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ilianza kazi yake .
Alisema
kadri masaa yalivyosogea asubuhi umbo lake liliongezeka na kutanuka kama vile
kinataka kulipuka na baadaye hali hiyo iliisha na baadhi ya wananchi
walianza kukisogelea na kukigusa kisha kujaribu kukihamisha
huku watoto na wanafunzi wakikinyofoa nyuzi zilizokifunika
Taswira
ya setelaiti iliyodondoka wilayani ngara.
Kwa upande
wake mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu alisema kutokana na kitu hicho
kuanguka eneo la wilaya yake lilisababisha taharuki kubwa kwa wananchi ambapo
baadhi yao waliamini kuwa ni kombora la masafa marefu lililorushwa kutoka
kutokana na vita vinavyoendelea kwenye nchi ya DRC dhidi ya waasi wa 23 na
majeshi la serikali.
Kamanda wa
polisi mkoani kagera Philip Karangi aliwataka wananchi wa ngara kushilikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kwa kutoa taarifa za kiusalama mapema
ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza badala ya baadhi ya wananchi kufanya
kazi za kitaalamu zisizowahusu hali inayoweza kusababisha madhara makubwa
kutokana na uzembe.
Kikosi cha
Brigedia ya Faru Makao makuu ya Tabora kinasimamia mikoa minane ya Kanda ya
ziwa ikiwa ni Tabora,Shinyanga,Simiyu,Mara,Mwanza,Geita,Kagera na Kigoma.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment