Na Daniel Limbe,Geita
WIKI moja baada ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Geita mkoani hapa kumkataa Daktari wa mifugo Thobias Kiputo kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kuwadharau na kufunga minada ya mifugo wilayani humo kwa
madai ya kuwepo ugonjwa wa miguu na midomo kwa lengo la kuikosesha halmashauri
mapato,madiwani hao wameendelea kuonyesha msimamo wao na kumtaka mkurugenzi wa
halmashauri hiyo kumwondoa wilayani humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisa utumishi wa halmashauri
ya wilaya ya geita Charles Kimaro wakati akiwasilisha taarifa ya ugawanywaji wa
watumishi na mali za halmashauri ya geita kwa lengo la kuzitenganisha
halmashauri tatu kiutawala kutokana na serikali kuanzisha halmashauri ya mji wa
geita na halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale.
Baada ya Kimaro kuwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha
baraza la madiweani kilichoketi leo ili kuivunja halmashauri ya geita na
kuanzisha rasmi halmashauri ya mji wa geita na halmashauri za wilaya ya
Nyang’hwale na Geita ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya madiwani
walionyesha kutaharuki kutokana na kuendelea kulisikia jina la Dk Kiputo.
Akichangia hoja ya ugawanaji wa watumishi,mali na madeni
ya halmashauri ya wilaya ya geita Diwani wa kata ya Nzera Joseph Musukuma
alisema kitendo cha kuendelea kusikia jina la Daktari huyo ndani ya orodha ya
watumishi wa halmashauri ni kutowatendea haki kwa kuwa tayari walikwisha azimia
kuondolewa kwa mtumishi huyo ndani ya wilaya ya geita.
“Mheshimiwa mwenyekiti ninasikitika sana kuendelea
kumsikia huyo daktari akiwa kwenye idadi ya watumishi wa halmashauri
yetu…tulisha mkataa na kamwe hatumtaki kwenye wilaya yetu…kama ni taratibu za
kisheria zifanyike lakini akiwa nje ya wilaya hii… kama hakuna pakumpeleka
mrudisheni alikotoka kabla ya kuja wilayani kwetu”alisema Musukuma kwa jazba
kali.
Kauli hiyo ilisababisha takribani madiwani watatu
kuchangia hoja hiyo huku wote wakionyesha msisitizo kuondolewa kabisa jina
Daktari huyo huku wakidai kuendelea kulisikia jina hilo nikuwadhihaki madiwani
hao kwa kuwa tayari walisha mkabidhi jukumu la kumfukuza kwenye halmashauri yao
.
Kutokana na hali hiyo
gazeti hili lililazimika kumtafuta Daktari huyo amnbapo alipuuza uamuzi huo na
kulazimika kuelezea sababu za baadhi ya madiwani hao kumkataa kuendela kufanya
kazi kwenye halmashauri hiyo kutokana na alichokisema kuwa baadhi yao wanamiliki
zabuni za kukusanya ushuru kwenye minada aliyoifunga kisheria baada ya kuwepo
ugonjwa wa miguu na midomo.
Aidha alifafanua kuwa pamoja na kumtuhumu kwa sababu
mbalimbali baadhi ya madiwani hao wanamiliki maduka ya kuuza pembejeo za kilimo
na mifugo licha ya kuwa hawana utalaamu wa kutoa huduma hiyo mhimu hali ambayo
imeonekana kuwapunguzia mapato.
“Lakini suala la kufunga minada ya mifugo ni la kitaalamu
zaidi…na taratibu za kufunga minada hiyo ilizingatia sheria taratibu na
kanuni…na ifahamike kuwa hayo hayakuwa maamuzi yangu binafsi isipokuwa ni agizo
la wizara husika ambayo iliazimia kuwekwa karantini ya kuchanja mifugo wote
waliopo geita ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo usilete madhara kwa
binadamu.
Hivi karibuni ikiwani Novemba 1 mwaka huu baraza la
madiwani wa halmashauri hiyo liliazimia kuondolewa kwa daktari huyo kwa madai ya
utendaji kazi wake kutokuwa na kulidhisha,kujibu jeuri kwa viongozi wenzake
pamoja na madiwani hao huku wakimtuhumu kumiliki kampuni ya kutoa chanjo ya
mifugo kwa maslahi yake binafsi.
No comments:
Post a Comment