WATOTO SABA WANUSURIKA KUFA CHATO.
Waziri wa ujenzi Dk John Mafufuli akitoa maagizo ya kukamatwa mhudumu wa afya.
Na Daniel Limbe,Chato
WATOTO
Saba wamenusurika kuawa kwenye hospitali ya wilaya ya Chato mkoani
geita baada ya mhudumu wa afya Maliagoreth Kyaruzi kuwanyofolea maji
yenye dawa (drip) wagonjwa waliolazwa kwenye wodi ya watoto kwa madai ya
ndugu zao kukataa kufanya usafi wa vyoo vya hospitali hiyo.
Watoto
walionusurika na vifo hivyo ni Edward Robert(4)mkazi wa kijiji cha
Nyamirembe,Kashinje Lukanya(12) mkazi wa Busaka,Iren Nasib(3)mkazi wa
Bwanga,Naomi Tumain(5) mkazi wa Kachwamba,Yunis William(3)mkazi wa
Kasala,Astelia Siajali(2)mkazi wa Kahumo na Alphonce Makolobelo.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea leo majira ya saa 2:30 asubuhi baada ya
mhudumu huyo wa afya kuwataka ndugu za wagonjwa wote walilazwa kwenye
wodi ya wanawake na watoto kwenda kufanya usafi wa vyoo kutokana na
kuwepo kwa uchufu unaodaiwa kusababishwa na wagonjwa wenyewe.
Wakizungumza
na Blog hii baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo William Masai na
Ester Misungwi wamesema hatua hiyo ilikuja baada ya ndugu za wagonjwa
kukaidi amri iliyotolewa na mhudumu huyo aliyewataka kuondoka ndani ya
wodi hizo na kwenda kufanya usafi kwenye vyoo vya hospitali hiyo.
Baada
ya wananchi hao kukaidi amri hiyo mhudumu huyo anadaiwa alilaejea na
kuanza kunyofoa maji yenye dawa yaliyokuwa yamening’iniziwa kwa wagonjwa
kwaajili ya matibabu kisha kuondoka ndani ya wodi hiyo huku
akiwataka watu walioumizwa na kitendo hicho kushitaki popote watakapo
ona panafaa.
Hatua
hiyo iliwalazimu baadhi ya ndugu za wagonjwa waliolazwa hospitalini
hapo kuutafuta uongozi wa haospitali hiyo kabla ya kuwasiliana na katibu
wa mbunge wa jimbo la Chato Gelvas Stephano ambaye naye alizungumza na
waziri wa ujenzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo ambaye alifika eneo
la tukio akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Magufuli alilazimika kuzungumza na wagonjwa,na
watumishi wa afya kwa lengo la kusikiliza kero zao muda mchache baada ya
kumaliza kujionea hali halisi ya watoto waliokuwa wamenyofolewa drip za
dawa kisha kulejeshwa baada ya ndugu za wagonjwa kulalamika.
Kutokana
na malalamiko mengi yaliyotolewa na wagonjwa kuhusu vitendo
vinavyofanywa na mhudumu huyo Waziri Magufuli amelazimika kumwagiza mkuu
wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo kwa kushirikiana na Jeshi la polisi
kuhakikisha wanamtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha afikishwe
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
“Bahati
nzuri mkuu wa wilaya upo hapa,na Ocd na wewe upo hapa…ninaagiza huyo
Maliagoreth akamatwe mara moja na kesho afikishwe mahakamani kujibu
tuhuma za kutaka kuuwa wagonjwa saba kwa makusudi”alisema Magufuli
“Nasema
huyo siyo mhudumu anayetakiwa kufanya kazi ya afya…maana kuwanyofolea
drip wagonjwa kwa kosa la ndugu zao kukataa kufanya usafi wa vyoo
haliwezi kufumbiwa macho….huyo maliagoreth hafai na ninaomba kuanzia leo
asikanyage hapa kwenye hospitali kuja kuhudumia wagonjwa…maana ipo siku
hata mimi ataninyofolea drip,naamini mmenielewa”alisema Magufuli na
kushangiliwa na wagonjwa.
Kadhalika
magufuli aliwataka waganga na wauguzi wengine kutoa huduma nzuri kadri
ya inavyopaswa na kuwatahadhalisha iwapo watawahudumia wagonjwa vibaya
kwa lengo la kulipiza kisasi kwa madai wagonjwa wamewashitaki kwake ambapo amedai
kufanya hivyo itakuwa ni kutowatendea haki wagonjwa.
Vilevile
amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Shaban Ntarambe
kuhakikisha anamsimamisha kazi mara moja nesi huyo kwa madai hana sifa
za kuendelea kuwa mtumishi kwenye wilaya ya chato.
Mkuu
wa wilaya ya chato Rodrick Mpogolo mbali na kudai kusikitishwa na tukio
hilo ameahidi kuunda tume maalumu itakayochunguza utolewaji wa huduma
za afya kwa wananchi wanaofika kutibiwa hapo kutokana na kuwepo kwa
malalamiko mengi.
Aidha
amesema msingi wa serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma
bora na kwamba dosari zinazojitokeza atahakikisha zinapatiwa ufumbuzi
wa kudumu ili kusijitokeza vitendo kama vilivyojitokeza.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Dk Pius Buchukundi amekiri kutokea
tukio hilo na kudai kuwa kitendo kilichofanywa na mhudumu wake siyo
msimamo wa hospitali bali ni matakwa yake mwenyewe na kwamba atahukumiwa
kwa matendo aliyoyatenda yeye mwenyewe.
Dk
Buchukundi amewataka wagonjwa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa
hospitali hiyo ili kila kunapojitokeza mapungufu kama hayo yaweze
kushughulikiwa haraka badala ya kukaa kimya na kuondoka wakinung’unika.